Abiri data ifuatayo
ya kiitariano kasha ubainishe yafuatayo:-
a.
[tinta]-rangi
b.
[ntɛnda]-hima
c.
[ntɛrɔ]-nyeusi
d.
[sapɔndɛ]-
sabuni
e.
[tiŋgɔ]-
napaka rangi
f.
[fuŋgɔ]-
uyoga
g.
[tɛŋgɔ]-
uyoga
h.
[bJaŋka]-nyeusi
i.
[faŋgɔ]-
matope
j.
[ɑŋkɛ]
I.
Je
kuna jozi linganuo finyu? Ni hitimisho gani unalolitoa kuhusu jozi hizo?
II.
Ni
kigezo kipi kinahusika na mtawanyo wa sauti [n] na [ŋ] katika data hii?
III.
Je
sauti [n] na [ŋ] ni alofani za fonimu moja au ni fonimu mbili tofauti?
IV.
Je
kuna kanuni yoyote inayoshika mtawanyo huo?
**************
i.
Je
kuna jozi linganuo finyu?
Ndiyo ipo jozi linganuo finyu kwa sababu kama anavyosema
Fischer (1957) anaeleza kuwa jozi linganuo finyu ni tofauti ndogo kabisa ya
kifonolojia iliyopo baina ya maneno fulani Aghalabu maneno hayo huwa yana:
Idadi sawa ya fonimu, mpangilio sawa wa fonimu ila unatofautishwa na fonimu mbili
ambazo zipo katika mazingira sawa ya utokeaji.
Hivyo kutokana na data tuliopewa kuna maneno yenye idadi
sawa na mpangilio sawa wa fonimu. Maneno hayo ni:-
[tiŋgɔ] na [fuŋgɔ]
[tɛŋgɔ] [faŋgɔ]
Hitimisho tunalotoa katika jozi hizi ni kwamba katika
lugha ya kiitaliano maneno haya [tiŋgɔ], [tɛŋgɔ], [fuŋgɔ] na [faŋgɔ] yana idadi
sawa ya fonimu na mpangilio sawa wa fonimu ila tofauti kidogo inayojitokeza
katika fonimu [i], [ɛ], [u] na [a].
ii.
Ni
kigezo kipi kinachohusika na mtawanyo wa sauti [n] na [ŋ] katika data hii?
Kuna vigezo viwili vinavyohusika na mtawanyo wa sauti [n]
na [ŋ] vigezo hivyo ni mgawanyo wa kimtoano na ufanano wa utofauti wa
kifonetiki.
Mgawanyo wa kimtoano ni dhana ambayo hutumiwa kuelezea
uhusiano uliopo baina ya sauti mbili au zaidi ambazo haziwezi kutokea katika
mazingira sawa, kama ilivyo katika maneno ya kiitariano katika data, [tɛŋgɔ],
[tiŋgɔ], [fuŋgɔ] na [faŋgɔ]. Mahali inapotokea sauti[n], sauti [ŋ] haiwezi
kujitokeza.
Mfanano wa kifonetiki ni sauti zinazofanana kifonetiki au
ni sauti zilizo na sifa bainifu zinazofanana. Kama ilivyo kwa [tinta], [ntɛnda],
[ntɛrɔ] katika data ya kiitaliano.
iii.
Sauti
[n] na [ŋ] ni alofoni za fonimo moja au fonimu mbili tofauti?
Sauti [n] na [ŋ] ni alofoni za fonimu moja kwa sababu
Mgullu (1999) anasema Alofoni ni matamshi tofauti tofauti ya fonimu moja. Kwa
asili neno hili ni la kigiriki Alo- ni tofauti tofauti na Foni -ni sauti.
Kwahiyo alofoni za sauti moja huunda kundi moja ambazo
hubadili maana ya maneno. Alofoni zote hufanana kisauti. Na mofimu ni kipashio
kidogo katika lugha ambacho kina sifa pambanuzi za kuweza kutofautisha vipande
vingine vya aina yake (Massamba 2004).
Hivyo sauti [n] na [ŋ] ni alofoni za fonimu moja kwa
sababu tunaona kuwa nazali /n/ inapofuatiwa na kitamkwa /d/ na /t/ hubakia kuwa
/n/. Pia nazali /n/ inapofuatiwa na kitamkwa /g/ hubadilika na kuwa [ŋ]. Hivyo
hii ina maana kuwa katika mazingira haya sauti /n/ na /ŋ/ ni alofoni za fonimu
jumuishi /N/ kwa mfano:-
[tiŋgɔ], [tɛŋgɔ], [fuŋgɔ] na [faŋgɔ].
iv.
Je
kuna kanuni yoyote inayoshika mtawanyo huo?
Ndiyo kuna kanuni inaoshika mtawanyo huu.
/N/→[α mahali]/-k
Kwa kuhitimisha tumeona kuna jozi linganuo finyu kama tulivyoona kwenye
data ya [tiŋgɔ], [tɛŋgɔ], [fuŋgɔ] na [faŋgɔ], vile vile tumeona kuna vigezo vya
ufanano na utofauti wa kifonetiki na mgawanyo wa kumtoano na fomula inayoshika
mtawanyo huo ni:-
/N/→[α mahali]/-k
MAREJEO
Massamba, D.P.B na Wenzake (2009), Fonologia ya kiswahili sanifu
( Fokisa),sekondari na vyuo,Taasisi ya uchunguzi wa
kiswahili:
Chuokikuu cha Dar es salaam.
Mgullu R.S (1999),Mtaala
wa isimu, fonetiki, fonolojia na mofolojia ya kiswahili: Longman
publishers(Kenya) Ltd.
Sahv kanuni imebadilika
ReplyDelete/N/->[π]/---K
Delete