Wednesday, May 7, 2014

Abiri data ifuatayo ya kiitariano kasha ubainishe yafuatayo:

Abiri data ifuatayo ya kiitariano kasha ubainishe yafuatayo:-
a.       [tinta]-rangi
b.      [ntɛnda]-hima
c.       [ntɛrɔ]-nyeusi
d.      [sapɔndɛ]- sabuni
e.       [tiŋgɔ]- napaka rangi
f.       [fuŋgɔ]- uyoga
g.      [tɛŋgɔ]- uyoga
h.      [bJaŋka]-nyeusi
i.        [faŋgɔ]- matope
j.        [ɑŋkɛ]

       I.            Je kuna jozi linganuo finyu? Ni hitimisho gani unalolitoa kuhusu jozi hizo?
    II.            Ni kigezo kipi kinahusika na mtawanyo wa sauti [n] na [ŋ] katika data hii?
 III.            Je sauti [n] na [ŋ] ni alofani za fonimu moja au ni fonimu mbili tofauti?
 IV.            Je kuna kanuni yoyote inayoshika mtawanyo huo?


 **************










                                i.            Je kuna jozi linganuo finyu?

Ndiyo ipo jozi linganuo finyu kwa sababu kama anavyosema Fischer (1957) anaeleza kuwa jozi linganuo finyu ni tofauti ndogo kabisa ya kifonolojia iliyopo baina ya maneno fulani Aghalabu maneno hayo huwa yana: Idadi sawa ya fonimu, mpangilio sawa wa fonimu ila unatofautishwa na fonimu mbili ambazo zipo katika mazingira sawa ya utokeaji.

Hivyo kutokana na data tuliopewa kuna maneno yenye idadi sawa na mpangilio sawa wa fonimu. Maneno hayo ni:-
[tiŋgɔ] na [fuŋgɔ]
[tɛŋgɔ]     [faŋgɔ]

Hitimisho tunalotoa katika jozi hizi ni kwamba katika lugha ya kiitaliano maneno haya [tiŋgɔ], [tɛŋgɔ], [fuŋgɔ] na [faŋgɔ] yana idadi sawa ya fonimu na mpangilio sawa wa fonimu ila tofauti kidogo inayojitokeza katika fonimu [i], [ɛ], [u] na [a].

                              ii.            Ni kigezo kipi kinachohusika na mtawanyo wa sauti [n] na [ŋ] katika data hii?

Kuna vigezo viwili vinavyohusika na mtawanyo wa sauti [n] na [ŋ] vigezo hivyo ni mgawanyo wa kimtoano na ufanano wa utofauti wa kifonetiki.
Mgawanyo wa kimtoano ni dhana ambayo hutumiwa kuelezea uhusiano uliopo baina ya sauti mbili au zaidi ambazo haziwezi kutokea katika mazingira sawa, kama ilivyo katika maneno ya kiitariano katika data, [tɛŋgɔ], [tiŋgɔ], [fuŋgɔ] na [faŋgɔ]. Mahali inapotokea sauti[n], sauti [ŋ] haiwezi kujitokeza.
Mfanano wa kifonetiki ni sauti zinazofanana kifonetiki au ni sauti zilizo na sifa bainifu zinazofanana. Kama ilivyo kwa [tinta], [ntɛnda], [ntɛrɔ] katika data ya kiitaliano.

                            iii.            Sauti [n] na [ŋ] ni alofoni za fonimo moja au fonimu mbili tofauti?

Sauti [n] na [ŋ] ni alofoni za fonimu moja kwa sababu Mgullu (1999) anasema Alofoni ni matamshi tofauti tofauti ya fonimu moja. Kwa asili neno hili ni la kigiriki Alo- ni tofauti tofauti na Foni -ni sauti.

Kwahiyo alofoni za sauti moja huunda kundi moja ambazo hubadili maana ya maneno. Alofoni zote hufanana kisauti. Na mofimu ni kipashio kidogo katika lugha ambacho kina sifa pambanuzi za kuweza kutofautisha vipande vingine vya aina yake (Massamba 2004).

Hivyo sauti [n] na [ŋ] ni alofoni za fonimu moja kwa sababu tunaona kuwa nazali /n/ inapofuatiwa na kitamkwa /d/ na /t/ hubakia kuwa /n/. Pia nazali /n/ inapofuatiwa na kitamkwa /g/ hubadilika na kuwa [ŋ]. Hivyo hii ina maana kuwa katika mazingira haya sauti /n/ na /ŋ/ ni alofoni za fonimu jumuishi /N/ kwa mfano:-
[tiŋgɔ], [tɛŋgɔ], [fuŋgɔ] na [faŋgɔ].

                            iv.            Je kuna kanuni yoyote inayoshika mtawanyo huo?

Ndiyo kuna kanuni inaoshika mtawanyo huu.
/N/→[α mahali]/-k
Kwa kuhitimisha tumeona kuna jozi linganuo finyu kama tulivyoona kwenye data ya [tiŋgɔ], [tɛŋgɔ], [fuŋgɔ] na [faŋgɔ], vile vile tumeona kuna vigezo vya ufanano na utofauti wa kifonetiki na mgawanyo wa kumtoano na fomula inayoshika mtawanyo huo ni:-
/N/→[α mahali]/-k







MAREJEO
Massamba, D.P.B na Wenzake (2009), Fonologia ya kiswahili sanifu
           ( Fokisa),sekondari na vyuo,Taasisi ya uchunguzi wa
                              kiswahili: Chuokikuu cha Dar es salaam.
Mgullu R.S (1999),Mtaala wa isimu, fonetiki, fonolojia na mofolojia ya kiswahili: Longman publishers(Kenya) Ltd.

1 comment: